Endo stories · Endometriosis

Safari Yangu Na Endometriosis

Jina langu ni Esther Mbugua – Kimemia. Mimi ni mwandishi na mwanzilishi wa Yellow Endo Flower na The Yellow Flower Initiative. Mashirika haya mawili huelimisha na kuwawezesha wanawake, wasichana na wazazi wao juu ya afya ya hedhi.

Kuligunduliwa kwamba nilikuwa na uugua ugonjwa wa Endometriosis nikiwa na miaka 19,hii ni baada ya kuteseka miaka sita kila nilipokuwa katika  vipindi vya kutokwa na hedhi.  Kila ilipofika wakati wa hedhi nilishikwa na maumivu yasiyoelezwa, hakuna daktari aliyeweza kueleza ni nini haswa kilichokuwa cha fanya niwe na maumivu makali. Hadi sasa nimeenda hospitalini kwa upasuaji mara  tatu. Mara  ya kwanza  ilikuwa kuchunguza kibofu cha mkojo wangu, ili wabaini kwa nini nilikuwa nikipata UTI mara kwa mara. Upasuaji wa pili uilikuwa laparoscopy, hapa ndipo waligundua endometriosis ilikuwa imeunganisha tumbo langu kubwa na ovari ya kushoto. Baada ya hapo nilipewa madawa kali ambayo yalinipa dalili za menopause. Upasuaji wa tatu ulikuwa kuondoa viambatisho na kuondoa kipengee changu pia.

Endometriosis ilinipigia ndoto zangu, kuna siku nyingi ambazo nilikuwa nimechoka sana,hata singeweza kuondoka kutoka kitanda changu. Endometriosis ilifurisha tumbo yangu na hewa au gasi nyingi  hadi nguo zangu zengine zilikuwa zinanikaaba sehemu ya tumbo. Maumivu makali pia ilimaanisha singeweza kufanya kazi yeyote. Nilikuwa ninajilaza juu ya sakafu ya tiles ili baridi ya tiles ipunguze maumivu.

Kila nilipokuwa katika vipindi vya hedhi nilikuwa na maumivu makali!  Maumivu ya mgongo, gasi au hewa mingi kwa tumbo, uchovu, kutokwa na damu nyingi nzito wakati wa hedhi, kuvimbiwa na tumbo au constipation kwa kingereaza, maumivu ya kichwa na kuhara.Maumivu  huwa yaweza kupata mwanamke ata kama hayuko katika kipindi chake cha hedhi. Kwa mfano, nilianza na kusikia maumivu tu wakati wa vipindi vyangu vya hedhi, kisha maumivu yakaanza kuja ata nikuwa na ovulate na pia siku chache kabla ya vipindi vya hedhi kuanza.

Nilisikia hadithi za ugomvi kabla ya kujua ukweli, la kwanza ilikuwa kwamba mwanamke akimpata mimba itaponya endometriosis. Kwa kweli kila wakati nilpokwenda kwa hospitali, niliulizwa kwa nini sikuwa na ujauzito. La pili ni kwamba mwanamke aliye na endometriosis aidha ako na mapepo ama amelaaniwa.

Nilikuwa nikibeba madawa mbalimbali za maumivu katika kibeti changu. Wakati maumivu yangekuwa makali sana, basi hapo ilibidii niende hospitali kupewa sindano ya kupunguza maumivu.

Mara ya kwanza,Madaktari walidhani kwamba nilikuwa na hali ya kibofu . Pale kibofu ilipopatikana kwamba haina shida ndipo madaktari waliendelea na matabibu yao hadi kupatikana kwa endometriosis.

Hakuna tiba inayojulikana ya Endometriosis. Upasuaji wa excision ndiyo kiwango cha dhahabu katika kutibu ugonjwa wa endometriosis . Kuna madawa mbalimbali ya homoni yaliyotolewa ili kusaidia kupunguza dalili za endometriosis na kupunguza maumivu. Madawa haya huchukuliwa kulingana na maelezo ya daktari, utumiaji ya haya madawa  hutofautiana kutoka kila siku au  kwa kila wiki au kila mwezi ikiwa sindano.

Wosia wangu kwa wanawake wanao ishi na ugonjwa wa endometriosis ni kuwa mtetezi wako mwenyewe. Anza kusikiliza mwili wako na kuelewa maamuzi na mifumo yake. Usiogope kutafuta maoni ya pili, na soma sana juu ya Endometriosis. Jiunge na kikundi cha msaada. Shirika la Yellow Endo Flower huwa na mkutano wa kundi la msaada mara moja kwa miezi miwili huku Mombasa. Shirika la Endometriosis Foundation of Kenya na Endo Sisters East Africa Foundation pia hutoa msaada kwa wanawake wanaoishi Nairobi na sehemu za bara.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s